Advertisement

Responsive Advertisement

KCMC YATUA TANGA KUCHANGISHA FEDHA ZA KITUO CHA TIBA YA MOYO

HOSPITALI ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini ya Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC), imeandaa hafla ya chakula cha jioni jijini Tanga, ambapo pamoja na mambo mengine, itachangisha fedha kwa ajili ya kukamilisha mradi wa ujenzi wa Kituo cha Tiba ya Moyo mkoani Tanga.


Jumla ya Shilingi bilioni 3 kati ya Shilingi bilioni 25 zinazohitajika kwa ununuzi wa vifaa tiba kwenye Kituo hicho, zinachangishwa kwa wadau mbalimbali katika mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga yenye wanufaika wa huduma bobezi na za kibingwa zitakazotolewa KCMC.



Ujenzi huo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuboresha sekta ya afya na upatikanaji wa huduma bora zenye viwango vya juu, kupitia uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu ya matibabu ya kibingwa na yale ya kuzuia magonjwa.


Mkuu wa Mkoa wa Tanga,  Dkt. Batilda Burian, amewaalika wadau wakiwemo wafanyabiashara, taasisi za umma na binafsi na watu wenye mapenzi mema, kushiriki hafla ya chakula cha jioni itakayofanyika Mei 30, 2026, ikihusisha pia uchangishaji fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Kituo hicho uliofikia asilimia 40.


RC  Dkt. Batilda amewahimiza wadau wa maendeleo katika ukanda wa Kaskazini na maeneo mengine ya nchi, kushiriki hafla hiyo, ikibidi hata kwa kupiga simu kwa uongozi wa Mkoa ama KCMC, ili kuwa sehemu ya kufanikisha mradi huo wenye taswira ya sadaka kwa maisha ya watu.


Kwa upande wa Tanga, Dkt. Batilda amesema hivi sasa mkoa huo unafunguka kama kitovu kikuu cha uchumi kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika, kutokana na uwekezaji mkubwa unaoendelea kufanyika.




Alisema, Kituo cha Tiba ya Moyo mkoani Kilimanjaro kitarahisisha upatikanaji wa huduma za kibingwa kwa urahisi na ukaribu zaidi, badala ya wakazi wa mikoa hiyo kusafiri umbali mrefu kwenda jijini Dar es Salaam.


Pia,  Dkt. Batilda alisema Kituo hicho kitapunguza rufaa zisizo za lazima kwenda Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) au hata nje ya nchi, na hivyo kuokoa gharama kubwa zinazotumiwa na wagonjwa. 


Naye Afisa Miradi na Mipango wa KCMC, Emmanuel Bianchi, amesema takwimu takribani asilimia 70 ya wagonjwa wanaopewa rufaa kutoka KCMC kwenda JKCI, wanashindwa kumudu gharama kutokana na changamoto zikiwemo za kijiografia na mahitaji kama malazi, usafiri na chakula.


Kwa mujibu wa  Dkt. Batilda, takwimu za Wizara ya Afya zinaonyesha kuwa asilimia 40 hadi 60 ya wagonjwa wanaokwenda JKCI, wanatokea mikoaya Kanda ya Kaskazini, jambo linalothibitisha uhitaji mkubwa wa kusogeza huduma hizi

Post a Comment

0 Comments