Advertisement

Responsive Advertisement

PM MWIGULU NCHEMBA AWAONYA WANAO TOA TAARIFA ZAKULETA TAHARUKI



Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewaonya Watanzania dhidi ya kuendelea kusambaza taarifa za uongo na ajenda zinazolenga kuleta taharuki nchini. 


Ametoa kauli hiyo leo Mei 23, 2026, wakati akizungumza na wananchi wa Iringa mjini. Akizungumzia mfululizo wa taarifa potofu zinazoenea mitandaoni, Dkt. Mwigulu amesema:


"Unakaa hivi sijui Padri katekwa, nimeona jana mtandaoni mtu katekwa, kaumizwa ana pingu, hizi ni ajenda maalum, hii ni michezo, na hii michezo haijaanza jana, na Watanzania tuamke. Hizi ni ajenda za watu wenye akili, naijua hii michezo."


Amefafanua kuwa baadhi ya matukio kama mauaji ya watu wasiokuwa na maslahi yoyote ya kimali katika eneo la Kibiti miaka iliyopita yalikuwa sehemu ya mpango mpana wa

kuichafua Serikali na kupotosha umma.


Aidha, Waziri Mkuu amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama

kuwa makini na njama za aina hiyo na kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa dhidi ya wanaotengeneza au kusambaza

taarifa za kupotosha.


Post a Comment

0 Comments