Advertisement

Responsive Advertisement

MWINYI ASEMA HANA NIA YA KUONGEZA MUDA WA URAIS

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi, amesitisha mijadala kuhusu kuongeza muda wa Urais wake na kusisitiza umuhimu wa kuendelea kuisimamia Katiba ya Nchi ipasavyo.

Rais Dkt. Mwinyi amesema kupitia majukwaa mbalimbali kumekuwa na mijadala na mapendekezo ya kuongeza muda wa Urais zaidi ya miaka 10 iliyowekwa kikatiba, ameeleza wazi kuwa hana nia hiyo na kwamba mjadala huo hauna tija.


Amesema viongozi wameapa kuilinda Katiba na kutekeleza

majukumu yao kwa ufanisi, huku akieleza kuwa kipindi kilichobaki cha uongozi wake ni cha utekelezaji mkubwa wa maendeleo, hivyo ameagiza mjadala huo kusitishwa mara moja.



Post a Comment

0 Comments